KAMATI YA FEDHA NA UTAWALA IMERIZISHWA NA MWENENDO WA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA AMALI (UFUNDI) ILIYOPO KATA YA IJANIJA
Ziara ya kamati ya fedha na Utawala ya Halmashauri ya Mji wa Nzega imefanyika kwa kukagua mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya Amali (ufundi) yenye thamani ya Tsh.bilioni 1.6 iliyopo kata ya Ijanija Kijiji cha makomelo ,tukio hilo limefanyika jana Tarehe 12 February 2025.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Nzega Mhe.Berbala Makono ndie alie ongoza ukaguzi huo ambapo baada ya kuzungukia majengo yote 15 ametoa pongezi na kurizishwa kwa mwenendo wa ujenzi wa Mradi huo.
Mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya Amali kwa Mji wa Nzega ni wa kwanza hivyo ukikamilika unaelezwa utaleta matokeo chanya kwa jamii.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017