• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
NZEGA TOWN COUNCIL
NZEGA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Nzega

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Origin
      • Ukubwa wa Eneo
      • Watu wa Eneo Husika
      • Hali ya Hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
      • Orodha ya Madiwani
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mkakati
  • Utawala
    • Muundo wa Tasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Miji, Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Takwimu, Usimamizi na Ufuatiliji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio Vya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
  • Huduma Mbalimbali
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha wa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Maadili
      • Ukimwi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kukutana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Miongozo
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

NZEGA MJI YAHAMISHA STENDI YA ZAMANI KUONDOA MSONGAMANO KATIKATI YA MJI

Tarehe Iliyowekwa: August 11th, 2018

HALMASHAURI ya Mji Nzega imefanikiwa kuhamisha mabasi yote ya abiria ambayo yalikuwa yakitumia Stendi ya zamani katika upakiaji na ushushaji wa abiria kutoka mjini kwenda katika eneo la Sagara ambalo lina ukubwa wa ekari 10 kwa ajili kuondoa msongamano katikati ya Mji .

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Halmashauri  kufanikiwa kuweka miundo mbinu yenye thamani ya milioni 277.7 ambayo imesaidia katika hatua za awali za ufunguzi wa Stendi  mpya ambayo itatoa huduma kwa magari ya abiria yanayopitia Mkoani Tabora na yale kutoka Mkoani hap.

Kauli hiyo ilitolewa tarehe 02.08.2018 na  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nzega  Ndugu Philemon Magesa wakati wa sherehe fupi za uzinduzi wa Stendi hiyo iliyopo kando kando ya barabara kuu ya kwenda Shinyanga na Singida na maeneo mengine .

Alisema kwa kuwa Nzega iko kwenye  njia panda, eneo la Stendi ya mabasi ya zamani lilikuwa dogo na kulifanya kushindwa kuhimili wingi wa mabasi yaliyokuwa yakitoka nje ya Nchi na yale ya mikoa mbalimbali ambayo yalikuwa yakipitia Nzega na kusababisha msongamano na karaha kwa wasafiri na watumiaji wengine wa barabara.

Mkurugenzi alisema baada ya kuona Halmashauri haiwezi kukamilisha kazi zote kwa wakati mmoja waliamua kutumia fedha hizo kidogo kuanza na hatua za awali za kujenga jengo la kupumzikia abiria, Kituo Kiodogo cha Polisi, vibanda sita(6) vya kukatia tiketi, vyoo na ofisi, vibanda vya askari , Mamlaka ya Usafirishaji Tanzania(SUMATRA) na kulipa fidia wananchi waliokuwa katika eneo ilipojengwa Stendi.

Mkurugenzi  alisema, kazi nyingine ilikuwa ni kujenga uzio wa nyaya kuzunguka eneo la stendi,vibanda vya askari wa usalama barabarani, wakusanyaji mapato ya Halmashauri, kuweka taa za mwanga wa jua katika Ofisi kwa ajili ya kuimarisha usalama nyakati za usiku .

Alisema gharama halisi ya kujenga  Stendi hiyo hadi kukamilika kwa kiwango cha juu kulingana na michoro ya ubunifu zinahitajika bilioni 7.7 ambapo kwa kutumia mapato ya Halmashauri ya ndani itachukua miaka 10 ili kukamilisha ujenzi wake.

Mkurugenzi alisema kutokana na kuhitajika fedha nyingi kukamilisha ujenzi wote limefanyika uamuzi wa kuandika andiko maalumu kwa ajili ya mradi huo na kuuwasilisha Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo limeshawalishwa Wizara ya Fedha na Mipango ili kuweza kupatiwa fedha za kukamilisha ujenzi wa mradi huo mapema.

Alisema mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wake kutaweza kusaidia Halmashauri  kuongeza uwezo wa kukusanya mapato yake na ndani na kuiwezesha  kuelekea katika kujitegemea.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi  alisema wako katika hatua ya mwisho ya kupata eneo lenye ukubwa wa ekari 15 kwa ajili ya kuweka maegesho ya magari ya mizigo ambalo nalo litasaidia kuingizia Halmashauri  mapato yake ya ndani.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alilitaka Jeshi la Polisi Wilaya ya Nzega kushirikiana na Halmashauri kuhakikisha wanaimarisha ulinzi katika eneo hilo saa zote kwa kuwa ni jipya na liko mbali na makazi ya watu. Upo uwezekano wa watu ambao sio wema wakatumia nafasi hiyo kutenda uovu wa aina mbalimbali ikiwemo kuwapora abiria.

Alisema uhalifu wa aina yoyote ukitokea unaweza kuwakatisha tamaa wasafiri na wawekezaji ambao wangependa kutumia Stendi hiyo jambo ambalo linaweza kusababisha mapato ya Halmashauri kupungua kutokana na wasafiri kuwa na hofu. .

Aidha Mkuu wa Mkoa alioutaka uongozi wa Halmashauri  kuhakikisha huduma mbalimbali kama vile vyoo na kuweka vifaa vya taka zinakuwepo ili kuepuka magonjwa ya mlipuko wakati wa masika.

Naye abiria kutoka Yelayela wilayani Urambo kwenda Dar es salaam Mashaka Maganga aliipongeza Halmashauri  kwa uamuzi wake wa kuihamisha Stendi kutoka mjini kuiweka eneo la Sagara kwani limesaidia kuondoa msongano sio tu magari hata abiria walikuwa wanapata shida kutokana na kuwa wengi katika eneo dogo.

Matangazo

  • FOMU YA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021 December 17, 2020
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA October 01, 2019
  • KOROSHO- ZAO LA KIMKAKATI July 23, 2020
  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA HALMASHAURI YA MJI NZEGA December 16, 2022
  • Onesha Yote

Habari Mpya

  • WALIMU 184 AJIRA MPYA WAPATA MAFUNZO ELEKEZI

    July 09, 2025
  • KITUO CHA AFYA KITENGWE KIMEKUWA MKOMBOZI KWA WAKAZI WA KATA YA MWANZOLI NA MAENEO YA JIRANI

    July 03, 2025
  • WATUMISHI WA MJI WA NZEGA WAPATA MAFUNZO YA E-UTENDAJI

    June 27, 2025
  • MJI WA NZEGA WAPATA HATI SAFI

    June 19, 2025
  • Onesha Yote

Video

JARIDA KITUO CHA AFYA ZOGOLO & BULUNDE SEKONDARI
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Matukio
  • Matangazo
  • Zabuni

Kurasa zinazofanana

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tabora RS
  • TAMISEMI
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)

    Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA

    Simu ya Mezani: +255677003373

    Simu ya Mkononi: +255677003373

    Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Binafsi
    • Mlalamikaji
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017