SHULE SITA MPYA ZA JENGWA MJI WA NZEGA
Katika kipindi cha Miaka Mitano ya Utawala wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Sekta ya elimu imepata mapinduzi makubwa na hivyo kuweza kuweka mazingira bora ya uandaaji wa nguvu kazi ya kesho.
Shule mpya zilizojengwa ni Pamoja na; Shule ya Sekondari Mbila, Shule ya Sekondari Hussein Bashe, Shule ya Sekondari Humbi na shule ya kwanza ya Amali Wilayani Nzega ijulikanayo kama Nzega Techinical Sekondary School.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya wilaya ya Nzega, imejengwa shule ya sekondari yenye ghorofa moja, yaani Hussein Bashe sekondari iliyopo maeneo ya Uwanja wa Ndege.
Shule hizi zimeongeza udahiri wa Wanafunzi kwa kiasi kikubwa na hivyo kuwapatia Vijana wengi wa Kitanzania fursa ya elimu katika mazingira tulivu.
Kwa Upande wa Elimu Msingi, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya juhudi imara za Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Bashe, zimejengwa shule mbili za Msingi. Shule hizo ni Pamoja na shule ya Msingi Utemini na Shule ya Msingi Uwanja wa Ndege.
Madarasa na matundu ya vyoo pia yamejengwa kwa wingi ili kuhakikisha hakuna hata mtoto mmoja anabakia nyuma katika suala la kutafuta elimu bora.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017