AJIRA MPYA HALMASHAURI YA MJI WA NZEGA WAASWA KUWA WAADILIFU
Watumishi wapya 53 wa kada mbalimbali walio ajiriwa hivi kalibuni wamepatiwa mafunzo mafupi ya utumishi wa Umma, mafunzo hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega uliopo eneo la Ipazi ,yakiongozwa na Mkuu wa Idara ya rasilimali watu Mji wa Nzega Bi.Leah Kibaki
lengo la mafunzo hayo yalikuwa nikuwaonyesha miongozo na mienendo ya Mtumishi wa Umma anavyo takiwa awe kwakua mtumishi wa Umma ni kioo cha jamii
Mkurugenzi wa Mji wa Nzega Ndg.Shomary Mndolwa akizungumza na watumishi hao amesema ,najua mnajua kuwa ajira ni ngumu hivyo umepata frusa hii nenda kafanye kazi kwa bidii na pia mjiepushe na kuiga mambo msio yaweza kwakua hapa kila mmoja anajijua kwao anamaisha gani ,vilevile mjiepushe na rushwa kwakua ukikamatwa mimi nitakuwa shahidi wako namba moja wakukufunga na waasa zingatieni haya alisema .
Yusuph Juma ,mwajiriwa mpya kama Afisa maendeleo ya Jamii alisema tunamshukuru sanaa Mkurugenzi wa Mji wa Nzega kwakuleta mafunzo hayo kwani yametujenga sanaa nahivyo tutaenda kuyafanya kazi kwa bidi alisema
Mafunzo hayo yalifanyika kwa siku mbili ambapo watumishi hao walikura kiapo cha Uadilifu tayari Kwenda kuwa tumikia Wananchi wa Mji wa Nzega kwa uadilifu na kujitoa
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017