Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji wa Nzega la Pitisha Bajeti ya Tsh.bilioni 26.4 kwa mwaka wa fedha 2025/2026
akiongoza Baraza la bajeti Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Nzega Mhe.Berbala Makono amewapongeza watalamu wa Halmashauri ya Mji wa Nzega kwa kuandaa bajeti inayo endana na mahitaji ya Halmashauri ya Mji wa Nzega.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe.Naitapwaki Tukai akiwandani ya kikao cha baraza la Madiwani cha bajeti amewapongeza watalamu kwa kuandaa bajeti yenye tija kwenye Halmashauri .
Na pia kapongeza kwakusimamia miradi ya maendeleo kwa umakini mkubwa mpaka Mji wa Nzega umekuwa wa mfano wa kuigwa na Halmashuri zingine hapa nchini
Baraza la Madiwani la bajeti la Halmashauri ya Mji wa Nzega limekuwa likitoa ushauri kwa watalamu na kupitisha bajeti kama lilivyo fanya juzi tarehe 26 Februari 2025 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega uliopo eneo la Ipazi
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017