HALMASHAURI ya Mji wa Nzega imefanikiwa kuvuka lengo la utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kutokana na mapato yake ya ndani kwa vikundi vya vijana na wanawake ilivyoyokuwa imekusudia ambapo imetoa milioni 161.6 ambayo ni sawa asilimia 104.5 katika mwaka wa fedha uliopita.
Hatua hiyo inatokana na Halmashauri kuwa imepanga kutoa mikopo kwa vikundi hivyo ya milioni 154.6 lakini ikafanikiwa kuvuka lengo.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega Philemon Magesa wakati Mkutano wa Baraza la Madiwani lililofanyika tarehe 31.07.2018
Alisema tumefanikwa kukopesha kupitia SACCOS milioni 116 kwa vikundi 67 vya wanawake na milioni 45.9 kwa vikundi 9 vya vijana.
Aidha Magesa alisema kuwa hadi kufika mwezi Juni mwaka huu jumla ya milioni 87.4 kati ya milioni 182.9 sawa na asilimia 47.8 zilikuwa zimerejeshwa na vikundi vya wanawake na vijana vilivyokopa.
Alisema kuwa baadhi ya vijana wamekuwa wagumu kurejesha mikopo ukilinganisha na wanawake ambao wengi wao wamekuwa waaminifu na warejesha vizuri mikopo.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula aliitaka Halmashauri kuwa makini katika utoaji wa mikopo kwa vikundi ili kuepuka upoteaji wa fedha hizo na kuzifanya zizungeke na ziwafikie vijana , wanawake na watu wenye ulemavu wengi kwa ajili ya kujiendeleza.
Alisema ni vema kutoa mikopo kwa vikundi ambavyo bado vinadaiwa na kuongeza ni vema wakopaji wakaelimishwa kuwa fedha hizo ni mkopo na sio ruzuku ili wawe na wajibu wa kuzitumia kwa makusudi wakiokopea na sio kufanya starehe.
Katika hatua nyingine Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji wa Nzega limemchagua kwa kura zote Diwani wa Kata ya Mbogwe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Kapaya Sozy kuendelea kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwa kipindi cha pili mfulululizo.
Diwani huyo alipata kura zote 14 zilizopigwa na Madiwani za Madawani waliohudhuria Baraza hilo huku Diwani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo naye akimuunga mkono mgombea pekee huyo.
Awali Mkurugenzi Mtendaji Magesa alisema kila mwaka wa fedha unapoisha wanalazimika kuchagua Makamu wa Mwenyekiti na ndipo walipoviandikia Vyama vya CCM na CHADEMA kuleta mapendekezo ya majina ya Madiwani ambao wangegombea nafasi hiyo lakini ni Chama cha Mapinduzi ndio kilijibu kwa kumpendekeza Diwani wa Kata ya Mbongwe kuendelea kutetea nafasi hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri William Jomanga alisema kuchaguliwa kwa kura zote kwa Diwani huyo kumeonyesha kuwa Madiwani wenzake wanayo imani kubwa kwake ya kutaka aendelea kumsaidia katika kuliongoza Baraza hilo.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017