MADIWANI HALMASHAURI YA NZEGA MJI WAFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO
Katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa katika viwango na kufuata utaratibu madiwani wa halmashauri ya Mji Nzega wamefanya ziara kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa ambapo wametembelea baadhi ya miradi kuona jinsi inavyotekelezwa
Miradi iliyotembelewa ni mradi wa ujenzi wa shule ya msingi Utemini na zahanati katika kijiji cha uchama
Katika mradi wa ujenzi wa shule ya msingi utemini uliogharimu Tshs 250,000,000 fedha toka mfuko wa EP4R kwa kujenga vyumba tisa vya madarasa, jengo la utawala,matundu manne ya vyoo vya walimu na matundu 26 ya vyoo vya wanafunzi.Mradi huu umekwisha kukamilika ambapo hadi sasa shule imekwisha sajiliwa kwa Namba. EM19826 na wanafunzi tayari wanaendelea na masomo.
Akizungumza katika ziara hiyo, Msimamizi wa mradi wa ujenzi, Mwl. Peter Charles amesema “Shule hii itasaidia kuondoa mrundikano wa wanafunzi katika shule ya msingi Imeli, ushirika na makomelo ambazo zinaizunguka kata ya utemini na kuondoa kero kwa wanafunzi kutembea umbali mrefu kujitafutia elimu”
Aidha katika mradi wa ujenzi wa zahanati mpya katika kijiji cha Uchama inayojegwa kupitia fedha za mapato ya ndani shilingi milioni 50 ambapo ujenzi wake bado unaendelea ambapo tayari paa limekwisha ezekwa.
Akizungumza katika ziara hiyo mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Nzega Bi. Belbara Makono ambaye aliongoza ziara hiyo ameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo na kumtaka mhandisi kuhakikisha jengo la zahanati linakamilika kwa haraka kama walivyoafikiana ili kuondoa kero kwa wakina mama wajawazito na watoto kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017