Na JAMES KAMALA
Sintofahamu ya kukatika katika kwa umeme na mgawo wa mara kwa mara imelilazimu Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Nzega kuiomba shirika la ugavi wa umeme nchini – Tanesco kuokoa jahazi.
Akiongea wakati wa kuhitimisha baraza hilo Mjini Nzega jana, Mwenyekiti wa Baraza hilo la madiwani Mhe. Belbara K. Makono alisema kutokuwepo kwa umeme wa uhakiki kunarudisha nyuma juhudi za wakazi wa mji wa Nzega kujikwamua kiuchumi na hivyo Tanesco ishughilikia suala hilo haraka sana iwezekanavyo.
“Vijana wamejiajiri kwenye shughulil zinazohitaji umeme kama vile saluni, uchomeleaji na nyinginezo, hivyo Tanesco wanapaswa kuhakikisha kuna umeme wa uhakika,” Alisema na kuogeza kuwa hali hii inakwamisha juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kuimarisha upatikanaji wa umeme na kuwaletea wakazi wa Nzega na Tanzania kwa ujumla maendeleo.
Mhe. Makono pia aliitaka Tanesco kuwa inatoa mapema taarifa ya kukatika umeme badala ya kukaa kimya ili wakazi wa Mji wa Nzega waweze kujua mapema na kujipanga jinsi ya kukabiliana na hali hiyo.
Awali, Diwani wa kata ya Nzega Mjini Magharini Mhe. Godfrey Malema, aliliambaia Baraza hilo kuwa Umeme umekuwa ukikatika katika zaidi ya mara saba kwa siku akidai kuwa licha ya kuchelewesha shughuli za kiuchumi, wakazi wa mji wa Nzega wamekuwa wakipata hasara kubwa kama vile kuungua vifaa vya ndani.
“Haiwezekani wilaya zote za mkoa wa Tabora na maeneo mengine ya tanzania yana umeme, lakini hapa Nzega tuko gizani na umeme ukirudi hautengemai. Tunaomba meneje TAnesco ajitathimini na ikiwezekana aondolewe,” alisema
Akiaongea kwaniaba ya Meneje tanesco wilaya ya Nzega bwana Masimino Swalo, Fundi umeme kutoka shirika hilo bwana Abilal Nkya, alisema sababu za kukatika katika ovyo kwa umeme wilalyani hap kumekuwa kukisababishwa na hujuma kwa mindombino ya tanesco.
Hujuma hizo, Bwana Bilal alibainisha kuwa ni pamoja na wananchi kukatakata nguzo, kuiba nyaya na hiivyo kusababisha shirka hilo kushindwa kutoa huduma kama ipasavyo. Hata hivyo, sababu hizo zilikataliwa na Madiwani wa baraza hio kuwa hazina mashiko na haziingii akilini kwa kuwa hakuna ushahidi wa kushikika unoweza kutolewa na tanesco.
(Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano serikalini Halmashauri ya Mji Wa Nzega, James kamala)
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017