MHE.HUSSEIN BASHE AKABIDHI TSH.MILIONI 8 KWA KIJIJI CHA IDUDUMO KWAAJILI YA UJENZI WA NYUMBA YA MGANGA
Tarehe Iliyowekwa: May 13th, 2025
MBUNGE WA JIMBO LA NZEGA MJINI MHE.HUSSEIN BASHE AKABIDHI TSH.MILIONI 8 KWA KIJIJI CHA IDUDUMO ZA UJENZI WA NYUMBA YA MGANGA
Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe.Hussein Bashe ametoa fedha taslimu kiasi Tsh.milioni 8 kwa kijiji cha Idudumo kata ya Mwanzoli kwaajili ya Ujenzi wa nyumba ya Mganga wa zahanati ya Idudumo.
Zoezi hilo lilifanyika jana tarehe 12 Mei ,2025 kwenye Kijiji hicho cha Idudumo na muwakilishi wa Mbunge wa jimbo la Nzega Mjini ambae pia ni Diwani wa kata ya Nzega Mjini Mashariki Mhe.Salimu Abdulkadril ambapo baada ya kukabidhiwa fedha hizo kwenye Kijiji hicho,
kijiji pia kikamkabidhi Mkurugenzi wa Mji wa Nzega Ndg.Shomary Mndolwa tayari kwa kuanza kwa ujenzi wa nyumba hiyo ya Mganga .
Hizi ni miongoni mwajitihada za Mhe.Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini kuhakikisha wakazi wa jimbo la Nzega Mjini wakipata furahi wakati wote