VIKUNDI 37 VYA HALMASHAURI YA MJI WA NZEGA VYA PATA MKOPO WENYE THAMANI YA TSH.MILIONI 400.
Hafla fupi ya kuvikutanisha na kukabidhi hudi vikundi 37 vya Halmashauri vilivyo pewa Mikopo wa bila riba wenye thamani ya Tsh.milioni 400 iliyo fanyika katika ukumbi wa CCM ulipo Nzega Mjini ,nakushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe.Naitapwaki Tukai
Kabla ya kukabithiwa hudi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Nzega alipata wasaa wakutoa neno kwa wanavikundi ambapo amewataka Kwenda kutumia fedha hiyo kwenye lengo mahususi tu nasivinginevyo maana tunatarajia mikopo hii ikawaletee faida ili mjikwamue kimaisha na pia mrejeshe kwa wakati ili na wengine wanufaike nazo
Nae mkurugenzi wa Mji wa Nzega Ndg.Shomary Salim Mndolwa amewaasa wana vikundi hao kuhakikisha fedha hizo wanaludisha kwa muda ulio kubaliwa kwakua kuna wavikundi vingine vinasubilia fedha hiyoo
Mmoja wa wanakikundi Richard joseph (35) kutoka katika kikundi cha Safina Group amemshukuru sanaa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutufanikishia fedha hizo kwaniamba ya wanavikundi wenzangu tuna mshukuru sanaa Rais na pia hata sisi tutahakikisha hatuendi kumwangusha kwenye swala zima la kuzifanyia kazi ilizituletee maendeleo na pia tunamuahidi tutaenda kuzirejesha kwa wakati alisema
Halmashauri ya Mji wa Nzega imekuwa ikitenga fedha asilimia kumi kwaajili ya kuvikopesha bila riba vikundi vyakina mama,vijana na watu wenye ulemavu ,hivyo vikundi vya Mji wa Nzega vimeanza kunufaika na fedha hizo za asilimia kumi .
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017