Kamati ya fedha na utawala imefanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa matundu kumi ya vyoo katika shule sekondari Nzega dogo ambapo ujenzi huo umegharimu kiasi cha Tsh.milioni 20 fedha za mapato ya ndani
Ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 100 ,kukamilika kwa ujenzi huo utasaidia kupunguza uhaba wa matundu ya vyoo ulio kuwa unawakabiri wanafunzi wa shule hiyo ambapo kabla ya hapo kulikuwa kunamatundu manne ambayo yanatumiwa nawanafunzi Zaidi ya 300.
Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti Bi.Berbala Makono imeishukru halmashauri kwa kuwajali wananchi wake na kusimamia vyema fedha ,huo nimwendelezo wa halmashauri kutumia mapato ya ndani katika kupeleka miradi kwa jamii.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017