Tumieni mifumo ya taarifa zamifumo ya GIS kufanya maamuzi yenye tija’ – OR TAMISEMI.
Halmashauri za Wilaya na Mji Nzega zimetakiwa kufanya maamuzi ya mbalimbali kwa kutumia mifumo ya taarifa za kijiografia (GIS) ili kutoa huduma kwa wananchi kwa haraka na kupunguza gharama za kiuendeshaji.
Akiongea katika mafunzo ya siku moja ya mwongozo GIS Mjini Nzega jumanne, Afisa Mipangomiji Mwandamizi Kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw.George Joseph Miringay, alisema ni wakati sahihi sasa kwa halmashauri hizi kuachana na mifumo ya kizamani ya kutumia taarifa za kiutawala ambazo hazina ufanisi zaidi
“Tayari kuna anwani za nyumba na makazi pamoja na ramani za maeneo, halmashauri hizi zinapaswa sasa kutumia taarifa za GIS ili kufanya maamizi ya kisayansi yenye tija kwa maendeleo ya wananchi na kupunguza gharama za kiutendajii,” alisema
Aliongeza kuwa manufaa ya kutumia taarifa za GIS katika kufanya maamuzi ni pamoja na kujua wapi pana umuhimu na uharaka wa kuelekezwa miundombinu ya Huduma za afya, shule na barabara ielekzwe, kuliko kuirundika sehemu moja na kulazimisha wananchi kusafiri mwendo mrefu kutafuta huduma hizo.
Kwa upande wa kupunguza gharama za kiutendaji, Bwana Miringay alisema kuwa matumizi ya taarifa za mifumo ya kijiografia zitasaidia halmashauri kujua ni watumishi gani wanatoka mbali na hivyo kustahili posho, na pia kujua kiasi gani cha mafuta ya gari yatahitajika kuzungukia Shule zote wakati wa ukaguzi au kusambaza mitihani
“Matumizi ya mfumo wa GIS pia utarahisisha ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha yanawasilishwa kikamilifu bila kupotea. Mfumo huu pia utasaidia kujua mipaka ya kiutawala na hivyo kusaidia kwa mfano kukabiliana na magonjwa ya milipuko kwa kuelekeza nguvukazi na rasilimali nyingie kwenye kiini cha magonjwa hayo,”
Alisema kuwa wadau wengine wa mfumo ya GIS ni pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Wakuu wa Mikoa yote nchini, Halmashauri za Wilaya, Kata, Mitaa au Vitongoji na pamoja na sekta binafsi.
Kwa upande, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Nzega Bwana Shomary Mndolwa alihahidi kutekeleza yote yaliyofundishwa kwa kushirikiana na Ofisiya Rais TAMISEMI. Bwan Mndolwa alisema kuwa nyaraka zote muhimu zitapitiwa na kufanyiwa kazi ipasavyo.
Imeandaliwa na kitengo cha habari serikalini,
Hamashauri ya Mji Nzega.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017