WATUMISHI KUTOKA VITUO VYOTE VYA KUTOLEA HUDUMA YA AFYA MJI WA NZEGA WAPEWA MAFUNZO
Watumishi kutoka vituo vya serikali na binafsi vya kutolea huduma ya afya wamepewa mafunzo ya kujenga uwezo wa kutoa huduma za afya bora kwakufata miongozo iliyo weka .
Mafunzo hayo yamefanyika siku ya Alhamisi na Ijumaa kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji Nzega uliopo oneo la Ipazi .
Mkufunzi wa Mafunzo hayo Daktari Benedict Komba kutoka ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa
amesema wataalamu hawa tunajua wanauwezo mkubwa wa maswala ya afya lakini kujifunza huwa hakuna mwisho hiki wanacho kipata hapa kitaenda kuwaongezea zaidi uwezo wa kutoa huduma ya afya bora kwakufata miongozo .
Daktari Anna Chanduo Mganga Mkuu Halmashauri ya Mji wa Nzega amewaasa wanamafunzo kuhakikisha wanasikiliza kwa makini kwakua wao pia watakuwa wakufunzi wakiludi kwenye vituo vyao vya kutolea huduma za afya
,na pia pale wataona hapaja eleweka ni vyema kuuliza ili kupata ufafanuzi alisisitiza hilo.
Henry Paul ni muuguzi wa Halmashauri ya Mji Nzega ambae pia alikuwa mshiriki kwenye mafunzo hayo amesema anaishukuru sanaa serikali kwakua inawakumbuka kuwaletea mafunzo ambayo yanasaidia katika kufanya kazi kwa ubora na kwakufuata miongozo.
Watumishi walio hudhulia kwenye mafunzo hayo nipamoja na wafawidhi wa vituo,Wauguzi,watalaamu wa maabara ,timu ya usimamizi na uendeshaji wa huduma za afya Halmashauri ya Mji wa Nzega na wafamasia .
Mafunzo yamendeshwa kwa siku mbili kuanzia siku ya Alhamisi na kumalizika siku ya Ijumaa baada ya mafunzo hayo kunatarajiwa ufanisi katika kazi utaongeza maladufu.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017