Na James Kamala, Afisa Habari, Nzega Mji.
Wakazi wa Wilaya ya Nzega wenye magonjwa sugu wanaendelea kupatiwa matibabu ya kibingwa katika hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Nzega. Lengo la kambihiyo ya kibingwa ni kuhudumia takribani wakazi 500 ndani ya siku tano zilizotengwa.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Nzega Dkt Anna Chaduo, alipoeleza kwamba madaktari bingwa tayari wapo na wanaendelea kutoa huduma kama ilivyopangwa.
Dkt Chaduo alisema madkatari wanaotoa huduma za kibingwa kwenye kambi ya siku tano,ni pamoja na madaktari bingwa wa Usingizi, daktari bingwa wa watoto, Upasuaji, njia ya mkojo, magonjwa ya ndani na wale wa akina mama.
“Ujio wa wataalamu hawa kwenye kambi ya siku tano unafaida kubwa kwa wananchi. Faida hizo ni pamoja na kupunguza gharama na usumbufu kwa wangonjwa ambao wangelazimika kwenda mwendo mrefu kufuata huduma hizi kwenye hospitali za rufaa nje ya Mkoa wa Tabora,” alisema.
Aliongeza kuwa mbali ya kutoa huduma za matibabu, wataalamu hao wenye ubobezi wa kutoa huduma za afya, watafanya kazi sambamba na madakatri wa hospitali ya Mji wa Nzega na hivyo, kuwapatia ujuzi zaidi wa kuwahudumia wagonjwa.
Dkt Chaduo alisema tayari serikali imesheleta mashine ya kusaidia wagonjwa wenye matatizo ya kupumua na nyinginezo, ambazo wataalamu hao watasaidia kuweleimisha watendaji wa hospitali yake jinsi ya kutumia mashine hizo na kuzitunza kwa ajili ya huduma za afya zenye tija.
Kambi hiyo ilianza siku ya jumatatu tarehe 10/06/2024 na itadumu hadi siku ya ijumaa tarehe 14/06/2024. Tayari wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega wamejitokeza kwa wingi ili kupata ushauri, vipimo na matibabu ya kibingwa.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017