Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri ya Mji wa Nzega wapata mafunzo ya mfumo wa IFT-MIS(Inspection and Finance Tracking Management Information System)
Mafunzo haya yameendeshwa kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega uliopo eneo la Ipazi ambapo yameongozwa na wakufunzi ambao ni mthibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Mji wa Nzega Ndg.Richard Majumbi,Mkuu wa kitengo cha TEHAMA Mji wa Nzega Ndg.John Mude Pamoja na Bi.Bridget Charles ambae ni Mhasibu wa Hoja
Aki shuhudia mafunzo hayo Mkaguzi wa ndani kutoka ofisi ya katibu tawala mkoa wa Tabora Bi.Elizabeth Paschal amesema lengo la mfumo huu wa( Inspection and Finance Tracking Management Information System ) IFT-MIS itaongeza uwajibikaji kwa watumishi wa Umma hususa katika kujibu hoja kwani Mfumo huu utamtaja mhusika wa hoja moja kwa moja ,pia itarahisisha utekelezaji wa hoja za CAG kwa wakati mbali na hivyo mfumo huu utakuwa na uwezo wakutunza kumbukumbu kila kitu kitahifadhiwa kwenye mfumo hivyo mambo yote yatakuwa kwenye mfumo alisema
Mshiriki wa mafunzo yao Emmy Mwansasu katibu wa Afya amefurahishwa na mfumo hu huku akisema utaenda kusaidia kupunguza ile mizunguko kwakua hoja itajibiwa kwenye mfumo na pia kama kutakua na changamoto italudishwa kwenye mfumo .
Hii nimiongoni mwa mbinu mbali mbali inayo kuja nayo serikali kuthibiti na matumizi mabaya ya fedha za serikali kwakua mfumo utakuwa unafatilia moja kwa moja matumizi ya fedha za serikali mpaka mwisho
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017