WAKUU WA IDARA ,VITENGO NA WATENDAJI WA KATA WAPATA MAFUNZO
Wakuu wa idara,vitengo na watendaji wa kata wa Halmashauri mbili yaani Halmashauri ya Nzega Mji na Halmashauri ya Wilaya wamepata mafunzo ya haki za binadamu ,utawala bora na usalama wanchi.
Mafunzo hayo yamefanyika jana kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega uliopo eneo la Ipazi na yalifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe.Naitapaki Tukai .
Katika kutoa hutuba fupi kwa Washiriki Mhe.Mkuu wa wilaya alisema “shirikini kikamilifu mafunzo haya nina Imani yatawasaidia katika kuleta chachu ya mabadiliko katika Kutenda haki niwaombe tena tumieni fursa hii ili mkawatendee haki Wananchi alisema ’’
Nae kaimu Mkurugenzi wa Mji wa Nzega Ndg.Ajalii Marumwengu amesema mafunzo haya yataleta tija katika kuwatumikia wananchi napia katika kuleta usawa hivyo mimi kwa nafasi yangu nitahakikisha walioko chini yangu wanatoa huduma kwakutenda haki kwani wamekubushwa na hakuna sehemu watasema wamesahau
Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku moja ni mwendelezo wa kampeni ya mamasamia ya msaada wa kisheria inayoendelea nchini ,ilikuwasaidia Wananchi maswala ya kisheria ,migogoro ya ardhi,unyanyasaji wakijinsia.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017