WATENDAJI WA INEC WAASWA KUWA WAADILIFU
Watendaji wa vituo wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mji wa Nzega katika uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura wameaswa kuwa waadilifu wakati wakiwahudumia wananchi watakao fika kwaajili ya kujaza au kuboresha taarifa zao
Akifungua mafunzo kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega uliopo eneo la ipazi mgeni rasmi Ndg.Shomary Salim Mndolwa amewaasa watendaji hao wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuwa waadilifu,kujiepusha na lugha chafu napia kujiepusha na ulevi kwani wasipo fanya hivyo watafanya zoezi hili lisifanyike kwa ufanisi hivyo kuingia katika mikono ya sheria nendani mkazingatie haya alisema
Mbali na maelezo hayo kutoka kwa Mgeni rasmi pia watendaji hawa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wamekula viapo vya kutunza siri na kujitoa Uanachama wa chama cha siasa ambapo kiapo hicho kimesimamiwa na Mhe.Nasra Mkandam Hakimu Mahakama ya mwanzo Nyasa
Mafunzo haya yanafanyika kwa siku moja na zoezi la uboreshaji linatarajiwa kuanzia 1 mei,2025 nakumalizika Tarehe 7 mei ,2025
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017