WAZIRI MKUU MHE.KASSIM MAJALIWA AFUNGUA STENDI KUU YA MABASI HALMASHAURI YA MJI WA NZEGA
Idadi kubwa ya wakazi wa Mji Nzega wamefurika kushuhudia tukio mhimu walio kuwa wakilisubilia kwa hamu la kufungua Stendi Kuu ya mabasi yaendayo mikoa mbalimbali na nje ya nchi .
Tukio hilo limetokea leo Tarehe 13 March 2025, kwenye eneo la stendi na limefanywa na Mhe Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ambapo alipata wasaa wa kuwa hutubia wakazi wa Mji wa Nzega huku akiwapa ushari wakuhakikisha wanatumia fursa ya kuwa wakazi wa Nzega kwakua Mji huu upo njia panda hivyo umekaa kibiashara mfanye biashara ili mjiingizie kipato
Pia amewataka wakuu wa idara na vitengo kuweka mpango mzuri wa kuifanya stendi iendelee kung’aa sio baada ya miezi kadhaa kuwepo na makopo na karatasi zinazagaa alisema
Stendi hii imetumia kiasi cha Tsh.bilioni 4 .3 Na imekamilika asilimia mia moja hivyo kufunguliwa kwake kunaenda kuifanya Halmshauri ya Mji wa Nzega iendelee kufunguka na kukua kwasi zaidi kuliko Halmashuari zingine hapa Nchini ,mhe Waziri Mkuu amehitimisha ziara yake katika Mji wa Nzega na kuelekea Halmashauri ya Wilaya Nzega
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017