Ziara ya mkuu wa wilaya nzega
Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mhe. Naitapwaki Tukai ameagiza wahandisi kuhakikisha miradi yote ya ujenzi midiradi ya huduma za kijamii wilayani huapa inakamilika kwa wakati ili kuharakisha huduma kwa wananchi.
Ameyasema hayo June 7,akifanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Mji wa Nzega huku akiongozana kamati ya ulinzi na usalama, kamati ya siasa ya Wilaya,pamoja na wakuu wa idara mbalimbali
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni ujenzi wa standi ya mabasi ya Sagara unaotarajiwa kumalizika mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu ,Mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari Husseni Bashe na jengo la mama na mtoto zahanati ya Miguwa.
Pamoja na miradi yote ya Boost ambapo kwa Halmashauri ya Mji Nzega ilipokea jumla ya shilingi milioni 984.5 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 12,matundu ya vyoo 18 pamoja na ujenzi vyumba 2 vya madarasa ya mfano yenye matundu 6 ya vyoo. Pia Halmashauri Ya Mji Nzega inatekeleza ujenzi wa shule mpya ya msingi ya mikondo miwili yenye ; jengo la utawala, madarasa 14, madarasa ya mfano 2 yenye matundu 6 ya vyoo, Kichomea taka, na matundu 18 ya vyoo vya wanafunzi. Mhe. Tukai ameagiza majengo hayo yakamilishwe kwa wakati lakini pia yaendane na thamani ya fedha iliyotumika, hivyo ubora na uimara wa jengo ni muhimu kuzingatiwa.
Akizungumza katika ziara hiyo Katibu wa Kamati ya siasa ya CCM Wilaya Bi.Adia Rashid amesisitiza wasimamizi wa miradi kuwa waaminifu na kuzitumia pesa za ujenzi kwa matumizi sahihi. Pia amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuipatia Halmashauri ya Mji Nzega miradi mikubwa ya maendeleo kama ujenzi wa standi mpya ya mabasi inayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.4 itakayosaidia kuongeza mapato ya ndani ya halmashauri.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017