WAZIRI WA NCHI OR-TAMISEMI MH.ANGELLAH KAIRUKI AFANYA ZIARA HALMASHAURI YA NZEGA MJI
Tarehe 21/11/2022,Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Mh.Angellah kairuki amefanya ziara katika halmashauri ya nzega mji kwa lengo la kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa yatakayopokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023,
Akiwa katika ziara hii Mh.Angellah Kairuki ametembelea katika shule ya sekondari nzega day na kufanya ukaguzi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa 6 na ofisi 2 za walimu yanayojengwa shuleni hapo kupitia fedha za kapu la mama ambapo kwa halmashauri ya nzega mji ilipokea kiasi cha Tsh.milion 120 ambapo kwa sasa mradi upo katika hatua ya uwekaji madirisha,milango,sakafu na upigaji plasta.
Akizungumza katika ziara hiyo mkuu wa shule ya sekondari nzega day Bi.Mwanakombo Martin amesema “madarasa haya yatasaidia kuondoa adha ya upungufu wa vyumba vya madarasa na ofisi za walimu, mlundikano wa wanafunzi wengi katika darasa moja na utoro pia.
Aidha, Mh.Angellah kairuki amemtaka mhandisi wa halmashauri anayesimamia ujenzi huo Bw. Issa Mwalima kuhakikisha majengo hayo yanajengwa kwa ubora na ufanisi mkubwa na kumalizika kwa wakati
Pamoja na ukaguzi wa miundo mbinu Mh. Angellah Kairuki amewapongeza wananchi kwa kushiriki katika hatua ya awali ya uchimbaji msingi wa majengo hayo na kuwaomba waendelee kushirikiana na serikali ili kuleta maendeleo kwa nchi yetu.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017